Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Hatimaye Nimegundua Mtoto si Wangu Baada ya Miaka 4. Mama Mtoto Anataka Kuniroga

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Huyu dada nlidate naye miaka kadhaa iliyopita kabla sijaoa.kipindi nadate naye kumbe nlimkuta na jamaa then akamwacha akawa nami.mi sikujua.

Baada tu ya miezi kama tisa hivi akanambia ana mimba yangu.sikuwa nmepanga kumuoa.na nlishamwambia mapema coz nligundua tunapishana mambo kadhaa.

Nikamhudumia akajifungua nikawa kila mwisho wa mwezi namtumia 400,000 baadaye nikawa namtumia 500,000 mpaka miezi 5 ago nilikuwa namtumia 700,000 na mtoto namlipia ada, nalipa kodi ya nyumba kwa mwaka pia.

Nlimnunulia gari ili mtoto asisumbuke katika usafiri nlimnunua IST baadaye akauza nikamwongezea nikamnunulia Mark X kama ambavyo alitaka.

Huyu mama akawa anazid kunisumbua anata niwe nampa mil.1.2 kwa mwezi kwa matunzo ya mtoto. Nikamwambia basi asubiri kwanza niweke mambo yangu sawa maana kuna ujenzi wa nyumba nyingine natakiwa nimalize ghorofa 3.

Akaanza vituko na kutishia kunipeleka ustawi wa jamii.mimi sikutaka kufika huko. Nikajibana miezi miwili nikampa 850,000 nazo anadai ndogo.mimi sina pesa si tajiri ntafanyaje?

Akawa hatosheki bado anataka sometime tukutane tu sex.nikawa namkatalia ananitishia kuwa atakuja kazini kufanya fujo.pesa nimpe na bado anilazimishe tu sex mimi sitaki.

Nina mke na watoto wawili nao huku natakiwa niwa take care. Nina watu nmewaajiri nao wana familia zao wanategemea waishi kupitia kazi zao.

Week iliyopita nilimchukua mtoto nikampeleka kwa dr wangu tupime DNA jumatano kanipa majibu. Mtoto si wangu. Anasema alipima mara tatu sehemu tofaut tofaut.

Nmesikitika sana. Kumbe yule dada alikuwa anajua akanibambikia mimi makusudi. Sasa jambo baya ni yeye kuwa greedy.nmemwambia tu aendelee na maisha yake mtoto ntaendelea mlipia ada ya shule.

Alianza kutuma msg nimsamehe na kunibembeleza.nikawa siwezi mjibu kitu.sasa anatishia kuniroga n.k kwa nini wadada mnakuwa wakatili hivi?

Maisha yenyewe haya mafupi sana kwa nini tena tufanyiane mtima nyongo? Nmehuzunika sana. Sababu inaonekana wanawake wengi sasa hawana mapenzi ya dhati.

Post a Comment

0 Comments