Hii Hapa Sababu ya Senzo Kutoka Simba Kutimkia Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



IMEELEZWA kuwa sababu zilizomwondoa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Senzo Mazingisa, ambaye Agosti 9 alitangaza kujiuzulu nafasi yake ndani ya klabu hiyo na ikielezwa kuwa amejiunga na Yanga SC ni kushindwana na waajiri wake wa zamani ambao ni Simba.
 Mhariri Mwandamizi wa Gazeti la Championi na mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Saleh Ally Jembe, akizungumza katika kipindi cha Front Page kinachoruka kupitia +255 Global Radio amesema kuwa moja ya sababu kuu zilizomwondoa Senzo katika Klabu ya Simba ni kwamba alishindwana na Simba kuhusu malipo ya mkataba wake mpya, kwani kiasi alichoomba kuongezewa, Simba waligoma kutoa.

"Kwanza ni kuwapongeza Yanga SC, lakini Simba SC wamepaniki sana, wanahisi Senzo ataondoka na Chama au Simba itayumba kimafanikio, Senzo ameikuta tayari Simba ina mafanikio, imekwenda Robo Fainali (CAF Champions League), ilikuwa imebeba ubingwa (VPL) mara  mbili, Senzo hakuwepo.
“Yanga SC wana haki ya kufurahi sana kwa sababu walikereka Morrison kwenda Simba SC, na ninasikia walikuwa na sherehe ya kujipongeza, lakini Yanga wanapaswa kujua kwamba Senzo siyo kocha wala mchezaji, hawezi kuleta mafanikio ndani ya muda mfupi, wampe muda.

“Simba SC wanasema kazi aliyokuwa anaifanya Senzo alikuwa ameshawatoa sehemu ambayo kuna vitu hawakuwa wanavijua, baada ya hapo hakuna mwendelezo wa vitu vipya vyote wanavijua lakini walikuwa tayari kuendelea kufanya naye kazi, inawezekana hii ndiyo sababu inayowauma.
“Senzo atasaidia vitu vingi sana Yanga kuiboresha timu. Leo nilikuwa nahesabu, sasa ni mwaka wa 21 kila inapofika wakati wa usajili Simba na Yanga inakuwa burudani na hii ndiyo raha kwetu sisi watu wa michezo. Ni lazima mmoja amuumize mwingine sijui kwa nini?
“Mo na Senzo walikwaruzana kidogo, Mo alikuwa anataka Senzo aonyeshe progress  (mandeleo) ya kwamba Simba ifanye nini baada ya muda fulani, iingize shilingi ngapi, tatizo timu zetu hapa nchini hazina target  (malengo) kuhusu mapato.
“Niliandika makala kwenye Championi, najiuliza usajili unaofanywa na Yanga, pesa anatoa GSM au Yanga? Kama ni GSM anatoa kama msaada au atalipwa na Yanga, kama atalipwa ni lini na kwa mfumo gani? GSM wana nia nzuri na Yanga lakini mambo hayaendi, Yanga wawe na plan (mpango wa kueleweka).

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad