8/06/2020

Ifahamu Kemikali Iliyoisambaratisha BeirutTAKRIBANI tani 3,000 za kemikali ya ammonium nitrate zilizohifadhiwa miaka sita iliyopita katika ghala zimeelezewa kusababisha mlipuko huo uliotokea katika jiji la  Beirut ambayo ni bandari na mji kuu wa  Lebanon siku ya Jumanne.

Lakini ammonium nitrate ni nini na kwa nini inaweza kuwa kemikali hatari?

Ammonium nitrate (NH4NO3) ni kemikali iliyo na umbo la madonge meupe ambayo hutengenezwa viwandani. Matumizi yake huwa ni chanzo cha naitrojeni kwa ajili ya mbolea, lakini pia inatumika kwa ajili ya kutengeneza vilipuzi kwa ajili ya migodi.

Kemikali hii hutengenezwa duniani kote na ni rahisi kuinunua. Lakini utunzaji wake unaweza kuwa tatizo, na kemikali hii imekuwa chanzo cha ajali kadhaa za viwandani miaka ya nyuma.

Ammonium nitrate ni hatari kwa kiasi gani?

Yenyewe ilivyo, ni salama, anasema profesa wa kemia, Andrea Sella, kutoka shule ya sayansi ya Chuo Kikuu cha London. Hata hivyo, ukiwa na kiasi kikubwa cha kemikali hiyo kwa muda mrefu, huanza kuoza.

”Tatizo ni kwamba kadiri muda unavyokwenda kemikali huanza kufyonza unyevu na hatimaye hubadilika kuwa mawe makubwa,” anasema. Hatua hii hufanya kemikali hiyo kuwa hatari zaidi, anaongeza, kwa kuwa inamaanisha kuwa ukitokea mshtuko itaenea kirahisi zaidi.

Kadiri inapoachwa muda mrefu, kuna uwezekano zaidi wa kuchafuliwa na vitu kama mafuta, anasema afisa wa intelijensia ya jeshi, Philip Ingram.

Inapotokea hali hiyo inaweza kusababisha athari kwenye kemikali.

”Hutengeneza joto lake yenyewe, na ikianza kufanya hivyo, inaendelea kutengeneza joto hilo kwa muda,” Ingram anasema. ”Hali hiyo baadaye inaweza kusababisha mlipuko mkubwa kama tulioushuhudia kwenye video ya kutisha kutoka mji wa Beirut.”

Kilichotokea mjini Beirut


Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya  saa kumi na mbili siku ya Jumanne. Mwandishi wa BBC aliyekuwa katika eneo hilo aliripoti miili ya watu waliokuwa wamekufa na uharibifu mkubwa unaoweza kuifunga bandari hiyo ya Beirut kwa muda.

Vyombo vya habari viliwaonyesha watu wakiwa wamenasa chini ya vifusi. Shuhuda mmoja alielezea mlipuko huo kuwa mkubwa, hali inayoweza kusababisha watu kuwa viziwi, huku picha ya video ikionyesha magari na nyumba zilizoharibiwa

Kwa namna gani gesi zinazotengenezwa huwa hatari ?

Kemikali ya ammonium nitrate inapolipuka, hutengeneza gesi ya sumu ikiwemo nitrogen oxide na gesi ya ammonia. Moshi wa rangi ya machungwa husababishwa na gesi ya nitrogen dioxide, ambayo huambatana na uchafuzi wa hali ya hewa.

”Kama hakuna upepo wa kutosha, huwa hatari kwa watu walio karibu na eneo la tukio,” anasema Prof Sella.


Hutumika kwenye mabomu?

Kwa mlipuko huo, ammonium nitrate imekuwa ikitumika na majeshi ulimwenguni kote kama vilipuzi. Pia, imekuwa ikitumika katika matukio kadhaa ya kigaidi,l ikiwemo tukio la mabomu la mji wa Oklahoma mwaka 1995. Katika tukio hilo, Timothy McVeigh alitumia tani mbili za ammonium nitrate kutengeneza bomu lililoharibu jengo la serikali na kusababisha vifo vya watu 168.

Tukio kama hili lilishawahi kutokea hapo nyuma?

Mwaka 1921, takribani tani 4,500 za ammonium nitrate zilisababisha mlipuko katika vinu vya Oppau, Ujerumani, na kusababisha vifo ya watu 500.

Ajali mbaya ya kiwandani katika historia ya Marekani ilitokea mwaka 1947 mjini Galveston Bay, jimbo la Texas. Takribani watu 581 walipoteza maisha baada ya tani zaidi ya 2,000 zilipolipuka kwenye meli ambayo ilitia nanga bandarini.

Tukio la karibuni ni la mlipuko wa kemikali hiyo na nyingine ambapo watu 173 walipoteza maisha katika bandari ya Tianjin Kaskazini mwa China mwaka 2015.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger