8/20/2020

Kisa usaliti wa Ray, Chuchu Hansy kuja na tamthilia yenye mkasa huo Mwigizaji wa filamu Tanzania, Chuchu Hansy amepasua kwamba usaliti aliofanyiwa na baba wa mtoto wake, mwigizaji mwenzake Vicent Kigosi ‘Ray’ umemuumiza na sasa ameamua kuachia tamthilia inayohusu mkasa huo.


Chuchu ametoa tuhuma hizo wakati akizindua tamthilia yake mpya iitwayo “Play Boy” ambayo itakuwa ikirushwa kupitia application ya SwahiliFlix.

“Tamthilia hii ni mjumuisho wa matukio ya kweli yaliyowatokea watu wangu wa karibu pamoja na mimi mwenyewe, na inahusu mwanaume ambaye anakuwa kwenye mapenzi na wanawake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.” ameeleza.

Chuchu anadai tamthilia hiyo ambayo pia imesheheni mastaa kibao wa maigizo wa zamani kama vile Waridi, Kelvin wa Kaole, Single Mtambalike Richie.

“Nimepata hamsa zaidi ya kuiachia wakati huu baada ya kusalitiwa, napitia maumivu ya mapenzi” amesema mwigizaji huyo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger