8/12/2020

Klabu ya Samatta kushusha mshambuliaji mwingineKocha wa Aston Villa, Dean Smith anamuwinda mshambuliaji Ollie Watkins kutoka Brentford akiwa kama chaguo lake namba moja kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Oktoba 5 mwaka huu. 

Dili hilo kama litakamilika litawagharimu kiasi cha paundi milioni 25, nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 amefunga jumla ya magoli 49 Championship.(Sky Sports)


Gareth Bale hataondoka Real Madrid msimu huu na sasa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 32 yuko tayari kusalia Real kwa miaka miwili kabla ya kuhamia klabu mpya. (Mirror)


Gareth Bale


Kingo wakati wa Manchester City Mhispania David Silva, 34, atajiunga na Lazio mkataba wake utakapomalizika mwisho wa msimu huu. (Guardian)David Silva


Kiungo wa kati wa Manchester City David Silva, 34, Kujiunga na Lazio

Klabu za West Bromwich Albion, Leeds na Fulham zilizopandishwa daraja katika ligi ya Primia zinawania kumsajili Ryan Fraser, 26, winga aliyeondoka Bournemouth mwisho wa msimu wa Juni kwa uhamisho wa bure. (90Min)


Chelsea wanapania kuiuzia AC Milan kiungo wao wa kati Mfaransa Tiemoue Bakayoko, 25 na tayari wamepunguza bai yake kufanikisha mpango huo. (Sun)Tiemoue Bakayoko


Chelsea wapko tayari kumuuza kiungo wao wa kati Tiemoue Bakayoko(Kushoto) kwa AC Milan

Real Madrid hawana mpango wa kumuachilia kiungo wao wa kati Dani Ceballos, 24, kuondoka klabu hiyo atakaporejea nyumbani kutoka Arsenal. (AS)


Leicester City wameonesha nia ya kutaka kumnunua winga wa Burnley Dwight McNeil,20. (Sky Sports – via Leicester Mercury)


Mshambuliaji wa Leicester Kelechi Iheanacho, 23, ananyatiwa na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce. (Fotospor – via Sport Witness)Kelechi Iheanacho


Mshambuliaji wa Leicester, Mnigiria Kelechi Iheanacho

West Ham wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu mkataba mpya ambao utamfanya mshambuliaji Michail Antonio,30 kuwa mmoja wa wachezaji watakaolipwa donge nono. (Mail)


Mshambulijai wa Lazio, Ciro Immobile anadai kuwa Newcastle aliwasiliana na ajenti wake hivi karibuni kujadili uwezekano wake kuhamia Ligi kuu ya England. Mtaliano huyo wa miaka 30 hata hivyo ameahidi hataondoka Lazio. (Goal)Mshambulijai wa Lazio, Ciro Immobile


Mshambulijai wa Lazio, Ciro Immobile

Klabu mbili za Ligi ya Primia na moja ya Bundesliga zinamtaka mchezaji nyota wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles. (Sky Sports)HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger