8/03/2020

Mabinwa wa kombe la shirikisho wapokelewa Dar kwa shangwe


Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Namungo Uwanja wa Nelson Mandela hivyo wamerejea na taji la Kombe la Shirikisho.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wamerejea rasmi mjini kuendeleza shangwe la ubingwa walioutwaa Sumbawanga.

"Mabingwa kama mabingwa tumerejea kuendelea na furaha kwa kuwa tumeshinda na tumerudi sasa kuendelea na furaha yetu Dar.

"Mashabiki ni ngao yetu kubwa wamekuwa nasi bega kwa bega hivyo mambo mazuri yanakuja na tunafuraha kufikia malengo yetu," amesema.

Wachezaji wa Simba wamepanda kwenye basi rasmi lililoandaliwa wakiwa na mataji mawili la Ligi Kuu Bara pamoja na Shirikisho wakiwa Kwenye msafara kuelekea Msimbazi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger