Makonda Akabidhi Rasmi Ofisi Kwa RC Kunenge, Asema Ataendelea Kumlinda na Kumtetea Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Aliekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Agost 03 amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Aboubakar Kunenge ambapo amesema ataendelea kusimama kidete kumlinda na kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli kwenye kila jambo kwakuwa ndio "Role Model" wake. 


Mhe. Makonda amesema anajisikia amani na furaha kwa kumaliza safari yake ya utumishi katika Mkoa wa Dar es salaam akiwa ameacha alama kubwa kwa jamii, taasisi na kugusa maisha ya mmoja mmoja. 


Aidha Mhe. Makonda amesema kwa sasa ataendelea kuwa mshauri mambo mbalimbali yenye kuleta maendeleo kwa mkoa na Taifa kwa ujumla kwakuwa yapo mengi aliyojifunza katika safari yake ya utumishi. 


Pamoja na hayo Mhe. Makonda amesema kwa sasa analo jukumu la kuendelea kuhakikisha Rais Dkt. John Magufuli anapata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu ikiwa ni pamoja na Wabunge na Madiwani wa Chama cha Mapinduzi CCM.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad