8/20/2020

Mbunge wa CUF Awapongeza CCM


Mbunge wa Tanga kupitia Chama cha CUF aliyemaliza muda wake, Mussa Mbarouk, amekipongeza Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanya maamuzi sahihi ya kutokuwarudisha wagombea waliotoka CUF na kutimkia CCM na kuacha Udiwani katikati kabla ya muda wao kuisha.Kauli hiyo ameitoa wakati wa mahojiano na EATV na kusisitiza kuwa kwa dhati ya moyo wake, anakipongeze Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa kuhakikisha watu hao hawarudi kwani hii itakuwa fundisho kubwa kwa watu wenye tabia za kuhamahama."Wanaosema CUF imekufa ni wale waliokuwa na nia ovu na chama chetu, sasa wametoka na kuhamia vyama vingine, wale walioenda CCM mnajua kilichowatokea maana wenye chao hawakukubali kukaribisha wageni kwa sababu wapo waliokipatia tabu chama chao,  mimi nawapongeza CCM kwa kuwapiga chini wale Madiwani waliotoka CUF na kuhamia CCM", amesema Mbarouk.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger