Mji Ambayo Wanaume Hukata Ngozi zao ili Zifanane na za Mamba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Nchini Papu New Guinea, sehemu ya mashariki ya kisiwa hicho cha pili kwa ukubwa duniani, asilimia 80 ya watu huishi vijijini na wengi sehemu zilizotengwa ambazo zina mawasiliano madogo na dunia. Hapa jinsi Mark Stratton aligundua ni kuwa tamaduni za jadi bado zinatumika.

Nyumba za kiroho au Haus Tambaran kando na mto Sepik kaskazini mwa Papua New Guinea ambapo misimu hutambuliwa kama wanyama.

Katika moja ya matambiko ya zamani zaidi duniani, wanaume wa Sepik migongo yao na mabega hukatwa kwa wembe na kuacha alama kubwa baada ya kupona kufanana na ngozi ya mamba.

Watoto wa kiume huletwa na wajomba kwenye nyumba za misimu kukatwa. Shughuli hii huchukua saa moja au masaa mawili hivi.

Ukiangalia miili ya wanaume iliyokatwa unaweza kuhisi machungu waliyopitia.

Watoto wengine hupoteza fahamu kutokana na uchungu wanapokatwa. Wanaume hucheza zumari na vidonda hufunikwa kwa mafuta ya mti na udongo mweupe wa mtoto kuvikinga kutona na uchafu.


"Baada ya kukatwa vijana hao wa kiume wanaweza kuishi kwenye nyumba za misimu wakijifunza mbinu tofauti za maisha kutoka wa wanaume wengine. Wanatapa ujuzi kuhusu misimu ya kijijini, jinsi ya kuvua samaki na jinsi ya kuwasaidia wake na familia," anasema Malingi.

Vipi mamba walikuja kuwa ishara ya misimu huko Sepik. "Mamba ni ishata ya nguvu, anasema Malingi. "Tunawaogopa lakini sisi hupata nguvu kutoka kwao." Ananiambia kuwa kuna imani kuwa watu wa Sepik walitoka kwa mamba na kuibuka kutoka mtoni na kutembea ardhini.

Vijiji vingi viko mbali na vigumu kufikika na havina mawasiliano na dunia. Wanaishi kwa kula chakula kinachojulikana kama Sago na samki. Mimea wanayotegemea kwa minajili ya kifedha ni miwa. Nguruwe hufugwa kwa sherehe kama za kafara na kama pesa za kutatua migogoro.

Hata hivyo tamaduni hiyo imetoweka kutoka kwa baadhi ya jamii zinazoishi karibu na mito. Eneo la Kaminimbit, safari ya nusu siku wa mashua, niliambawa kuwa ukatajia huo wa ngozi umesitishwa kutokana na ushawishi wa wa kanisa la kikiristo. Baada ya utawala wa Ujerumani mwaka 1885 eneo la Sepik lilianza kupata injili.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad