8/12/2020

Mwamuzi apigwa ngumi ya uso na mchezaji kisa kadi nyekundu England, ahofia kumshitakiMwamuzi mmoja amepigwa ngumi usoni katika mchezo wa kirafiki baada ya kumpatia kadi nyekundu mchezaji wa klabu ya Sporting de Mundial mjini London siku ya Jumapili.


Refa akionesha kadi nyekundu


Maafisa wa polisi na wale wa huduma ya ‘ambulance’ waliitwa ili kuingilia kati. Mwamuzi huyo kwa jina Satyam Toki, 28 anafanya uamuzi wa kufikiria kuwasilisha mashtaka mahakamani.


Klabu hiyo ya Sporting de Mundial inasema kwamba mchezaji huyo ameondolewa katika timu hiyo na kwamba atapatiwa matibabu ya kiakili.Satyam Toki


SatyamToki ni mkufunzi na refa

”Tunashutumu kitendo hicho cha kutisha”, waliongezea katika mtandao wao wa Twitter.


Toki alisema kwamba alimuomba mchezaji huyo mara kadhaa kutumia lugha nzuri na kuwacha kulalamika, kabla ya kumuonya.


Alianza kutoka na kuelekea katika eneo la wachezaji wa ziada wa timu yake na alipokuwa akiondoka alinitishia kwamba ataniona baada ya mechi, Toki alisema.


”Ni wakati huo ndipo nilimpatia kadi nyekundu na kunipiga ngumi usoni”. Karibu anisababishie upofu kwa sekunde chache, na baadaye nilianza kutokwa damu.Satyam Toki


Toki anasema kwamba ana wasiwasi kwamba iwapo atamshtaki mchezaji aliemshambulia, huenda akapoteza kazi yake, lakini akaongozea kwa upande mwengine, iwapo sitamshtaki, katika siku za usoni huenda akamfanyia kitendo hicho mwamuzi mwengine.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger