8/12/2020

Watano mbaroni kwa utapeli wa kutumia majina ya Taasisi za Salma Kikwete na Mo Dewji Foundation
Watu watano mkoani Mwanza wamefikishwa mahakamani wakishitakiwa kwa jumla ya makosa 16 ikiwemo kujipatia fedha zaidi ya shilingi milioni 10 kwa njia isiyo halali na kufanya utapeli kwa kutumia majina ya taasisi za mama Salma Kikwete na Mo Dewji Foundation kwenye mitandao ya kijamii.  

Wakisoma mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mhakama ya Mkoa wa Mwanza Boniventure Lema, Mawakili wa Serikali Robert Kidando na Jackline Nyautu waliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Raphael John Kipingiri, Werasoni Tabu Ngedenge, Luck Paschal Paul, Musa Michael Masami na Richard Masalu Richard.

Mawakili walisema watuhumiwa hao wanakabiliwa na kesi namba 12 ya uhujumu uchumi ya mwaka 2020 kwani kwa nyakati tofauti walitenda makosa ya kula njama na kufanya uharifu, kujirasimisha uongo, kujipatia fedha kwa nia isiyo halali, kutumia taarifa za wateja vibaya kwenye usajili wa laini pamoja na utakatishaji fedha na uhujumu uchumi.

Walisema uchunguzi umebaini kuwa watuhumiwa hao walishiriki kufanya utapeli ikiwemo kutumia majina ya taasisi ya mama Salma Kikwete na Mo Dewji Foundation kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook na kufanikiwa kufanya utapeli na kutumia taarifa za vitambulisho vya watu wengine kukamilisha usajili wa laini za simu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, hakimu Boniventure Lema aliwataka washitakiwa wote kutokujibu chochote kutokana na makosa yao kuwa ni ya uhujumu uchumi ambapo kesi hiyo iliahirishwa na watuhumiwa walirejeshwa rumande mpaka agosti 26 mwaka huu ambapo itasomwa tena.

Akizungumuza nje ya mahakama baada ya kesi hiyo kusomwa Mkuu wa Mashitaka Mkoa wa Mwanza, Custuce Ndamugomba alikemea vikali tabia ya watu kutumia majina ya watu wengine kwenye mitandao ya kijamii kufanya utapeli na kuahidi kuwashughulikia ipasavyo watu wa aina hiyo.

Pia Custuce aliwashauri watanzania kutopenda kujipatia fedha na kazi kwa njia ya mkato kwani matapeli wengi hufanikisha adhima yao kutokana na watu wengi kujipatia pesa kiurahisi hali inayowafanya watapeliwe na hivyo alitoa wito kwa kila mtanzania kuwa makini na kutojiweka karibu na watu wa aina hiyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger