8/17/2020

"Mwana Fa ni Mtu na Nusu" - Shetta


Ni miaka 10 ya msanii Shetta kwenye muziki wa BongoFleva ambapo leo ametoa historia kuhusu msanii Mwana Fa kumsaidia kufanya nae wimbo wake wa kwanza baada ya kukataliwa na wasanii wakubwa huku wengine wakitaka awalipe pesa nyingi. Akieleza hilo baada ya kuandika ujumbe kuhusu kusaidiwa na Mwana Fa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Shetta ameeleza kuwa  "Story yangu fupi kuhusu Mimi na Mwana Fa, watu wengi hawajui kuwa Binamu yetu Hamis Mwijuma ndiyo msanii wa kwanza kabisa kufanya naye wimbo wangu wa kwanza na kunitambulisha kwenye muziki miaka 9 iliyopita ikiwa bado msanii mchanga, wimbo huo unaitwa mena play"

"Wasanii wakubwa walikuwepo wengine walikataa na walitaka niwalipe pesa nyingi, mimi  sikua na pesa kipindi kile lakini Mwana Fa alinipa muda wa kunisikiliza, mtihani alionipa ni kwamba kama wimbo utakua mkali atafanya na mimi ila kama mbaya basi tuendele kuwa mtu na mdogo wake hatofanya" ameongeza

"Baada ya kusikiliza wimbo huo moja kwa moja alikuja studio na akaingiza sauti, alipomaliza nikataka kumpa hela kidogo ya usumbufu japo ya mafuta akakataa, kiukweli Mwana Fa ni mtu na nusu, nimejifunza mengi na naendelea kujifunza kutoka kwake vitu vingi, kiukweli namkukubali sana"
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger