8/17/2020

Roma Mkatoliki Ajitokeza na Kuu Ukana Wimbo wa Lissu Shujaa Uliyowekwa Mtandao wa Youtube


Roma Ameandika Haya:'

Wimbo Wangu Wa Mwisho Kuutoa Ulikuwa Ni #Mkombozi Feat. @onesix1 Niliutoa January 3rd, 2020

Wimbo Wetu Wa Kundi (ROSTAM) Wa Mwisho Kuutoa Ulikuwa Ni #KakaTuchati Feat. @onesix1 @atan_africa @iamkarmatz Ulitoka May 9th, 2020.
.
Wimbo Wangu Wa Mwisho Kushirikiswa Ni #NALIA By @feroozgram Umetoka July 29th, 2020.

Kwa Mwaka Huu 2020 Mpaka Sasa Sijatoa Wimbo Wowote Ule Zaidi Ya Hizo!👆

Kuna Wimbo Unasambaa Mitaani na Kwenye Mitandao Ya Kijamii Nimeona Watu Wengi Wakinitaja Wakisema Wimbo Huo Nimeuimba Mimi, Nimeona Hata Picha iliyowekwa Kwenye Cover Ya Wimbo Huo Ni Picha Yangu Mimi!(Swipe Left👉👉)Na Wameandika Kuwa Ni Wimbo Wangu!

Naomba Nichukue Nafasi Hii Kuwatangazia Kuwa WIMBO HUO SIJAIMBA MIMI, NA WALA ILE SIO SAUTI YANGU MIMI, NA WALA SINA MAHUSIANO WALA SIMFAHAMU MTU ALIYEIMBA, NA WALA SIJAHUSIKA KWENYE UZALISHAJI WA WIMBO ULE,NA PIA STUDIO YANGU @tongwerecords HAIJAHUSIKA KWA LOLOTE KUHUSU WIMBO HUO!

Nasikitika Sana Ninapoona #Mashabiki #Wafuasi #Media Mpaka #Viongozi Mbali Mbali WakiniTag Na Kunipigia Simu Na Kuniambia Nimeimba Mimi Wimbo Huu!Nakuwa Dissapointed Kuona Ndani Ya #Miaka13 Niliyowahudumia Kwenye #Music Wanashindwa Kutambua Sauti Yangu Na Aina Ya Uandishi Wangu Na Vina Vyangu Na Flow Yangu!

Nafahamu Sana Inawezekana TumewaInspire Vijana Wengi Kufanya Sanaa Lakini Nafikiri Ni Vema Na Faida Kwao Wakatumia #Identity Zao Ili Wapate Wafuasi Wao Na Kutengeneza FanBase Yao Pia, ili Wayaone #Matunda Na #Changamoto Za Career Yao!

Mimi Nyimbo Zangu Zote Huwa Natoa Kupitia Platform Zangu (Mnazijua Mlionifata Huko) Na Kupromote kupitia Social Media Zangu(Mnazijua Mlioni-Follow)
.
.
Kwa Niaba Ya Studio Yangu Ya @tongwerecords Tunapenda Kuwaambia Mashabiki Wetu Kuwa Hatuhusiki Na Production Wala Maudhui Ya Wimbo Ule, Na Hatuwafahamu Watu Hao, Ambao Wamejaribu Ku-Sample Beat Yetu Ya Wimbo Wa #Roma Wa #MechiZaUgenini Kwenye Wimbo Wao Huo!!
.
.
Samahani Kwa Mashabiki Zangu Na Yoyote Aliyekwazika Na Hiko Kilichotokea!!
.
.
#NB: Siku #Roma Au (ROSTAM) Wakitoa Wimbo Nchi Nzima Itajua Kuwa Sasa Shughuli Ndiyo Imeanza!! Kwa Sasa Hatujatoa Bado #KuweniNaSubira
.
Nisaidie Kusambaza Ujumbe Huu
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger