Simba kuivaa Vital'O ya Burundi Simba Day

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kikosi Vital'0 ya Burundi kinatarajia kutua jijini, Dar es Salaam siku ya Ijumaa majira ya saa tano asubuh kwaajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba , kwenye tamasha la Simba Day litakalo fanyika Agosti 22, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.



Akizungumza na Waandishi a Habari,Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema walipanga kucheza na Al Ahly lakini changamoto ya Corona imefanya mpango huo kushindikana

"Tunaamini Vital'O itatupa changamoto nzuri kwenye mchezo huo kutoa wachezaji wengin wanaocheza timu ya Taifa Burundi lakini pia wachezaji wengine wanaocheza ligi ya hapa nyumbani"amesema Haji Manara.

Kwa upande mwingine Manara amesema katika kilele cha Simba day ,Jumapili hii kutakuwa na burudani nyingine hivyo kawaomba mashabiki wa Klabu yao kujitokeza kwa wingi ili wapate kuwashuhudia nyota wao wapya akiwemo Bernad Morrison na wengineo.

"Simba Day burudani itatolewa na Twanga Pepeta, Tunda Man, Meja Kunta, Mwasiti na kipekee atakuwepo Diamond Platinumz ,litakuwa kama tamasha la mziki, amekusudia kufanya jambo kubwa na kwa kupitia hilo kesho alhamisi kutakuwa na BIG SURPRISE kwa Wanasimba. MC atakuwa Mpoki"- Manara.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad