Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Simba Watwaa Ubingwa wa Kombe la Shirikisho 2020

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Klabu ya soka ya Simba imekamilisha msimu kwa kutwaa kombe la tatu baada ya leo Agosti 2, 2020 kushinda ubingwa wa Kombe la Shirikisho nchini kwa kuifunga Namungo FC magoli 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga.


Katika mchezo huo wa fainali Magoli ya Simba yamefungwa na Luis Miquissone dakika ya 27, John Bocco dakika ya 39 huku lile la Namungo FC likifungwa na Edward Charles Manyama dakika ya 56.

Luis Miquissone ameibuka mchezaji bora wa mchezo wa fainali na kukabidhiwa tuzo yake.Kwa ujumla msimu huu Simba walianza na Kombe la Ngao ya Jamii kwa kuwafunga Azam FC kisha wakatwaa ubingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania bara na sasa wamemaliza kwa Kombe la Shirikisho.

Simba sasa ni Mabingwa wa Kombe la Shirikisho kwa mara ya tano ambapo wamechukua mwaka 1984, 1995, 2000, 2017 na 2020.

Post a Comment

0 Comments