Ticker

6/recent/ticker-posts

Tabia ya Wadada/Wanawake Kubadilisha Status Kwa Hitilafu Ndogo za Kwenye Uhusiano

Leo naomba tujadiliane hili maana nimekua nikiliona sana,
Kwa ushahidi mkubwa nimeliona kwa rafiki zangu wengi sana na hata mimi limewahi kunitokea.

Mdada uliyenae uhusiano mkipishana kauli kidogo na ukawa kimya basi atadhani ndo keshapigwa chenga hapo ataanza kuhangaika na kubadilisha status kwenye social networks kama whatsapp, Facebook etc.

SHINDA ZAWADI YA SIMU KWA KUDOWNLOAD APPP YA UDAKU SPECIAL HAPA
Kwa mfano mlipokua kwenye uhusiano hajawahi kuandika jambo la hivi ila leo mnakwazana jambo dogo utaona Whatsapp au Facebook ameandika: AM SINGLE AND HAPPY, I CAN MANAGE MY LIFE, NAMTEGEMEA MUNGU TU SIO MWANADAMU.

Tatizo linalonikwaza ni kwamba kitendo cha mtu kuandika haya ni kuonyesha watu wengine kua hana siri juu ya mambo yake, yaani likimkuta tu lazima aropoke kwa kuweka status ya ajabu.

Huu naona kama utoto sana watu tujifunze kua na adabu ya kutunza privacy zetu

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments