8/16/2020

Urusi Yaanza Kuzalisha Chanjo ya Corona kwa Matumizi ya UmmaUrusi imeanza uzalishaji wa chanjo mpya ya ugonjwa COVID-19.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Interfax, likinukuu wizara ya afya.

Urusi inasema chanjo hiyo iliyogunduliwa na taasisi ya Gamaleya na kuwa ya kwanza kutengenezwa, itazinduliwa mwishoni mwa mwezi huu.

Tarehe 11 mwezi huu Rais Vladmir Putin wa Russia alitangaza kuwa, nchi yake imegundua chanjo ya kwanza kabisa ya virusi vya corona inayotoa kinga ya kudumu dhidi ya virusi hivyo.

Putin alisema kuwa tayari binti yake mmoja amepewa chanjo hiyo inayozuia maambukizi ya virusi vya corona na maradhi ya COVID-19.

Zaidi ya watu 21,385,925 wameambukizwa virusi vya corona kote duniani. Marekani inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya waathirika na watu walioaga dunia kutokana na virusi hivyo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger