9/24/2020

Ajibu Ajibu Mapigo ya ChamaKIUNGO mzawa ndani ya Simba, Ibrahim Ajibu, amejibu mapigo ya kiungo mwenzake, Clatous Chama kwa kutoa pasi ya mwisho ya kisigino iliyoleta bao ndani ya Simba.


 


Septemba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, Chama alitoa pasi ya kisigino kwa Chris Mugalu ambaye alifunga bao wakati Simba ikishinda 4-0 ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City. Dakika ya 85.


Baada ya Chama kufanya balaa hilo, Ajibu ambaye hajawa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza msimu huu, juzi Jumanne alipata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa kirafi ki dhidi ya African Lyon uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar.


 


Kwenye mchezo huo ambao Simba ilishinda 2-0, Ajibu alicheza dakika zote 90 na kumlipa Chama kwa kutoa pasi ya kisigino iliyozaa bao la pili lililofungwa na Mugalu dakika ya 46.Kwa sasa Simba inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC unaotarajiwa kuchezwa Septemba 26, mwaka huu Uwanja wa Mkapa.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger