Dkt. Hamisi Kigwangalla akutana na Balozi wa Marekani Dkt.Donald Wright kuzungumzia Utalii .

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( kulia) akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright kuelezea mafanikio ya Tanzania katika Uhifadhi wa Maliasili na utayari wa Tanzania kupokea Watalii kutoka  mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani wakati huu wa janga la Corona. Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam. 



 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( kulia) akimwomba Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright (kushoto) asaidie kuwahamasisha raia wa Marekani na watu maarufu wakiwemo Wasanii wakubwa wa Marekani  na vilabu mbalmbali maarufu vya michezo  vitembelea vivutio vya utalii vya Tanzania alipokutana nae kwa mazungumzo mafupi jijini Dar es salaam. 



 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( kulia) na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright (kushoto) Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo mafupi yaliyolenga kukuza Utalii hasa wakati huu wa janga la Corona na kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani katika shughuli za uhifadhi. 



 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( katikati) akitoa ufafanuzi kwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright (kushoto) na ujumbe wake kuhusu namna Tanzania ilivyofanikiwa kulinda maeneo yaliyohifadhiwa, kudhibiti ujangili pamoja na Taifa kuendelea kunufaika kimapato, kutoa fursa za ajira na uwekezaji kwa  Watanzania na Wageni akimwomba Balozi huyo asaidie kuhamasisha raia wa Marekani waje kuwekeza nchini Tanzania. 



 Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright (kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) walipokutana kwa  mazungumzo mafupi yaliyojikita katika kuimarisha ushirikiano na uendelezaji wa shughuli za uhifadhi baina ya Tanzania na Marekani leo  jijini Dar es salaam. 



Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla kuhusu mchango wa Taifa la Marekani katika shughuli za Uhifadhi nchini Tanzania na namna nchi yake itakavyoendelea kusaidia shughuli za uhifadhi katika eneo la Mafunzo, Teknolojia na Vitendea kazi  walipokutana kwa  mazungumzo jijini Dar es salaam.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad