9/21/2020

Ghorofa yaporomoka na kusababisha vifo IndiaWatu wasiopungua 10 wamefariki na watu 11 wamejeruhiwa kutokana na kuporomoka kwa jengo la gorofa nne nchini India.

Jengo la ghorofa nne limeanguka asubuhi katika wilaya ya Thane ya Mumbai, mji mkuu wa jimbo la Maharashtra.


Satya Pradhan, mkuu wa Kikosi cha Kitaifa cha Kukabiliana na Maafa, ameripoti kuwa watu wasiopungua 10 wamefariki na 11 wamejeruhiwa kutokana na kuanguka kwa jengo hilo.


Imeelezwa kuwa timu za utaftaji na uokoaji zimejaribu kuwafikia watu 20 hadi 25 ambao walikuwa wamekwama katika jengo hilo lililoporomoka.


Ni kawaida kuona majengo ya zamani yakiporomoka kwa sababu ya mvua za masika, haswa mnamo Juni na Septemba nchini India.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger