Maafisa wawili wa polisi wapigwa risasi wakati wa maandamano mjini LouisvilleMaafisa wawili wa polisi wamepigwa risasi huku maelfu ya watu wakiandamana katika mji wa Louisville baada ya jopo la mahakama kuamua kwamba hakuna mtu atakayeshtakiwa na mauaji ya Breonna Taylor.

Bi Taylor , mwenye umri wa miaka 26 , mfanyakazi mmoja wa hospitali alipigwa risasi mara kadhaa baada ya maafisa wa polisi kuvamia nyumba yake tarehe 13 mwezi Machi.


Brett Hankison ameshtakiwa, sio kwa kifo cha Taylor lakini kwa kuhatarisha maisha baada ya kufyatua risasi katika nyumba ya jirani yake huko Louisville.


Naibu afisa mkuu wa polisi Robert Schroeder amesema kwamba hali ya maafisa hao haipo hatarani . Aliongezea kwamba mmoja ya washukiwa amekamatwa. Hali ya tahadhari imetangazwa mjini Louisville na walinzi wa kitaifa pia wamepelekwa katika eneo hilo.


Meya Greg Fischer ameweka masharti ya kutotoka nje katika mji huo kwa siku tatu. Awali alikua amesema kwamba ametangaza hali ya tahadhari kutokana na uwezekano wa kuzuka wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE