9/24/2020

Mbwana Samatta Atua FenerbahceSamatta alijiunga na Aston Villa mwezi Januari mwaka huu kwa ada ya Euro 10.5 milioni akitokea KRC Genk


 Muda mfupi ujao, nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta atakamilisha uhamisho wa kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki.


 Samatta anayejiunga na miamba hiyo ya Uturuki kwa mkopo akitokea Aston Villa, jana saa 6 usiku kwa muda wa Tanzania, alitua katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Istanbul, Uturuki tayari kukamilisha usajili huo.


 Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo na mitandao mbalimbali ya habari, Samatta anajiunga na Fenerbahce kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja ambao utakuwa na kipengele cha kununuliwa moja kwa moja ikiwa kiwango chake kitairidhisha timu hiyo. 

 Mwandishi wa habari wa mtandao maarufu wa goal.com Ronan Murphy jana usiku alithibitisha kuwa Samatta ametua rasmi jijini Istanbul kwa ajili ya kumalizana na Fenerbahce.


 Kabla ya taarifa hizo za kutua kwa Samatta, ukurasa wa Twitter wa klabu ya Fenerbahce uliweka picha ya ndege inayotua na chini yake kukawa na peni inayoandika, inayoonesha walikuwa wakiashiria kuwa kuna mchezaji mpya anatua ili ajiunge na timu hiyo.


 Nafasi ya Samatta ndani ya Aston Villa imeonekana kuwa ngumu katika miezi ya hivi karibuni kutokana na takwimu zisizoridhisha alizonazo tangu alipojiunga na timu hiyo mwezi Januari mwaka huu.


 Samatta ameifungia timu hiyo mabao mawili tu katika mechi 16 za mashindano tofauti aliyoichezea tangu alipojiunga nayo huku akiwa hajapiga hata pasi moja iliyozaa bao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger