9/03/2020

Mbwana Samatta: Siondoki Aston VillaNAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, ataendelea kukipiga katika klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England.

Aston Villa imenusurika kushuka daraja msimu huu, baada ya kumaliza nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 35. Timu hiyo ilifanikiwa kubaki baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na West Ham inayofundishwa na kocha David Moyes.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Samatta alisema anajivunia kubaki Ligi Kuu England kwa msimu mwiTanzania

“Nataka kumshukuru Mungu kwa kunipa nafasi nyingine tena, napenda kuwashukuru mashabiki waliokuwa nyuma yangu, kuiombea Villa kubaki msimu ujao, nawaomba waendelee kuomba ili na mimi niendelee kubaki hapa,” alisema Samatta.

Samatta alijiunga na klabu ya Aston Villa akitokea Genk ya Ubelgiji kwa kitita cha pauni milioni 8.5 (zaidi ya sh bil. 25 za Tanzania).

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger