Mgombea wa Chadema Tundu Lissu, aahidi kubadilisha mfumo wa kodi nchini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu leo Septemba 14, 2020, katika kampeni zake zilizofanyika katika Mji wa Makambako amesema Serikali  ya chama hicho ikiingia madarakani itaondoa utitiri wa kodi na kuzuia ukandamizwaji  wa wafanyabiashara.



Mgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu.


Lissu amesema hayo wakati akinadi sera zake na kuahidi kuwa, atahakikisha wafanyabiashara ambao kweli wana madeni wanawekewa utaratibu mzuri wa kulipa ili wasiathiri biashara zao, lakini pia amesema ataboresha mahusiano ya Kimataifa yenye kuleta tija katika uchumi.


“Kuwa na deni sio ishu, kama unanilazimisha nilipe deni ili watoto walale njaa kwa sababu tu ya deni hiyo sio sawasawa,kama unataka nilipe deni ili biashara yangu ife hiyo sio sawasawa”, amesema Lissu.


“Kwahivyo tunaweka utaratibu kwa wafanyabiashara wenye madeni wataweza kulipa madeni yao bila kuua biashara zao”, ameongeza


Aidha mgombea huyo amesema kuwa atafanya mabadiliko makubwa ya mfumo mzima wa ulipaji kodi  ili kuhakikisha unaendana na maslahi ya wananchi.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad