9/03/2020

Rasmi: Manchester United Yamsajili Van De Beek


Klabu ya Manchester United ya England imekamilisha usajili wa Mchezaji Donny van de Beek (23) kwa ada ya Paundi Milioni 40 kutokea Klabu ya Ajax ya Uholanzi.

Van de Beek amesaini kandarasi ya miaka mitano kukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi na inaaminika atalipwa Paundi 107,000 kwa wiki pamoja na marupurupu.Huu ni usajili wa kwanza wa Kocha Ole Gunnar Solskjaer kwa dirisha hili la usajili ambapo Van de Beek anatarajiwa kutengeneza Kiungo kizuri katika timu hiyo pamoja na Paul Pogba na Bruno Fernandes.

Solskjaer anadaiwa sasa anaangalia uwezekano wa kusajili walau Beki mmoja wa Kati na Kiungo Mshambuliaji wa upande wa kulia huku Jadon Sancho akiwa ndio chaguo namba moja katika eneo hilo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger