9/23/2020

Shilole Avunja Ukimya Kupora Mume wa MtuMAMBO ni Moto! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya hivi karibuni, msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni mjasiriamali, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amevunja ukimya baada ya kuposti picha akiwa na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake wa sasa, kisha kuibua taharuki kama yote.


 


Miezi kadhaa baada ya kutemana na aliyekuwa mumewe, Ashraf Uchebe, wiki iliyopita Shilole aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram, ikimuonesha akiwa na mwanaume anayefahamika kwa jina la Rommy3D.


 


Mara tu baada ya kuposti picha hiyo, ndipo wenye ubuyu wakaibuka na kudai kuwa, huyo ndiye mwanaume wake mpya, lakini wakaenda mbali zaidi na kudai kuwa, amepora mume wa mtu. Watu wa karibu wamesema kuwa, huyo Rommy3D, awali ilifahamika kuwa ni mpigapicha wake, lakini kwa sasa inasemekana ni mume wa mtu.


 


Kufuatia madai hayo, kumeibuka mtafaruku kwa baadhi ya mashabiki wa Shilole mtandaoni, ambapo wapo wanaomshambulia na wengine kumtetea.


 


“Hee wanawake sisi hatujiheshimu kabisa, Shilole kwa kuiba waume za watu yupo vizuri. Uchebe alikuwa mume wa mtu, akamchukua, huyu naye ni mume wa mtu na unaambiwa sasa hivi Rommy anaishi kwa Shilole na amempa mkewe talaka tatu,” alidai shabiki mmoja aliyejiita Mama-Kuja, huku wengine wakimtetea na kumpongeza Shilole kwa kile alichokifanya.


 


“Ni mwendo wa kuvua gamba na kuvaa gwanda, Shishi Baby hana masihara kabisa. Uchebe alidhani amemkomesha, kumbe amejikomesha mwenyewe, mjini ukishakuwa mzuri, hakuna kinachokusumbua,” alisema shabiki mwingine aliyejiita Sabri.


 


MKE WA ROMMY ANENA


Ili kujua ukweli juu ya jambo hili, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilimtafuta mke halali wa Rommy, ambapo alisema kuwa, yeye hajaona habari hizo kwenye mitandao kuhusiana na mume wake kutoka na Shilole.


 


“Jamani mimi sijaona hizo habari wala nini na kwa nini mje mniulize mimi hayo mambo? “Kwa nini msiwaulize wahusika? Naombeni mniache, nipo mazoezini,” alisema mke wa Rommy kisha akakata simu.


 


SHILOLE AVUNJA UKIMYA


Gazeti la IJUMAA WIKIENDA halikuishia hapo, kwani lilifanya juhudi za kumsaka Shilole, ambaye ndiye mtuhumiwa kwenye ishu hii. Shilole alipopatikana, alivunja ukimya kwamba, hakuna kitu cha ajabu hapo, kwani hayo ni mambo ya kawaida tu.


 


“Mbona ni mambo ya kawaida, cha ajabu ni nini hapo? Niulizeni mambo ya maana kuhusu kazi zangu,” alisema Shilole kisha akaingia mitini. Ikumbukwe kwamba, miezi michache iliyopita, kulitokea sintofahamu kati ya Shilole na Uchebe, ambapo Shilole alidai kupokea kichapo kutoka kwa jamaa huyo, jambo ambalo lilisababisha wawili hao kutengana na jamaa huyo kufikishwa mahakamani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger