SOMA Hii Story Unaweza Ukajifunza Kitu Katika Maisha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kijana mmoja alisafiri kwa meli na rafiki zake,
wakiwa katikati ya safari yao meli ilianza
kuzama. Watu wengi pamoja na rafiki wa yule
kijana walikufa maji wakati wanajaribu kujiokoa
kwa kuogelea, lakini yule kijana alifanikiwa
kushika ubao ulioelea majini akaanza kuelea nao,
maji yalimpeleka hadi kisiwa cha mbali sana
ambako hakukuwa na watu wala wanyama
isipokuwa wadudu tu! Alifika ufukweni amechoka
sana na asiyeamini tukio lililotokea, akaishi huko
kwa kula matunda. Aliweza kujenga ka-kibanda
kwa shida sana maana hakuwa na shoka wala
panga, hatimaye akaanza maisha mapya.

Aliishi muda mrefu kisiwani na tayari alishazoea
mazingira yale ya shida japo shida haizoeleki.
Mara zote nyakati za jioni aliwasha moto kwa
kupekecha vijiti. Siku moja kama kawaida yake
aliwasha moto nje karibu na kibanda chake, aliota
moto muda mrefu hatimaye akapitiwa na usingizi.


Alilala hapo hapo hadi usiku wa manane
aliposhtushwa na joto kali lisilo la kawaida.
Kumbe moto ulishika nyasi za kibanda chake na
kibanda chote kikaungua moto.Alilia sana na
kumlaani sana Mungu kwa mateso hayo akisema
"Hivi Mungu nimekukosea nini mpaka unitese
hivi? Pamoja na shida zote hizi bado
unaniongezea shida nyingine, umeteketeza makazi
yangu ilhali nimejenga kwa shida, Hukuridhika
kunitenga mbali na familia yangu nilipoishi kwa
raha? Hukuridhika kuwaua rafiki zangu wote
baharini? Kwanini Mungu umekuwa mkatili hivi?
Bora nife tuu maana nimeshachoshwa na hizi
shida!" akaendelea kulalamika na kumlaani Mungu
hadi kukapambazuka.

Ilipofika asubuhi aliiona meli ikija kwa mbali
kuelekea alipo, alishangaa maana hakuna meli
yoyote inayoweza kwenda kisiwa kile labda kama
imepotea njia. Meli ilipofika ufukweni yule kijana
akaifuata, alienda moja kwa moja hadi kwa
kapteni.Kapteni akamwambia "tuliona moto mkali
sana usiku tukahisi ni meli inawaka moto
tukasema tuje ili tutoe msaada..kwa kweli
tumetembea masaa mengi sana hadi kufika hapa,
mshukuru Mungu maana ametumia moto kutuleta
hapa" yule kijana kusikia hivyo alilia sana,
akajilaumu kwa jinsi alivyo mnung'unikia Mungu.
Akaelewa kuwa Mungu ana njia nyingi za kuleta
msaada kwa mtu. Akapiga magoti akatubu huku
akimshukuru Mungu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad