9/28/2020

Uchebe Sasa Kocha Black Leopards SauzPATRICK AUSSEMS  aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba SC, ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Black Leopards inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu.

Aussems ambaye ni raia wa Ubelgiji aliwahi kuifundisha Simba SC na AC Leopards, alipigwa chini mazima na Simba msimu wa 2019/20 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwa kusimamia nidhamu ndani ya kikosi hicho.

Akiwa Simba aliweza kutwaa taji ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19 na alifanikiwa kukiongoza kikosi hicho kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Anatarajiwa kuwasili nchini Afrika Kusini wiki ijayo kwa ajili ya kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kipya.

Aussems ameiambia City Press kuwa :”Muda mrefu nilikuwa nahitaji kufanya kazi Afrika Kusini, nina furaha ya kupata kazi huko ninaamini nitafanya vizuri.

“Ligi ya Afrika Kusini imekuwa kubwa na ni maarufu ukianzia kwenye miundonbinu mpaka ukusanyaji wa taarifa na timu imeonekana ikipambana hivyo nitakwenda nayo sawa.”

Msimu wa 2019/20, timu hiyo ilimaliza Ligi Kuu ya Afrika Kusini ikiwa nafasi ya 15 na pointi zake 29 baada ya kucheza mechi 30.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger