9/29/2020

Wakili wa Idris Ashindwa Kufika MahakamaniMsanii na mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Idris Sultan, ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhairisha kesi namba 60/2020, inayomkabili pamoja na wenzake wawili ya kuchapisha maudhui mtandaoni bila leseni baada ya wakili wake kushindwa kufika mahakamani.


Mbali na Idris Sultan, washtakiwa wengine ni mfanyabiashara Doctor Ulimwengu (28) mkazi wa Mbezi Beach na Isihaka Mwinyimvua (22) ambaye ni msanii na mkazi wa Gongolamboto.


Idris Sultan ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Yusto Luborogwa, ambapo amesema kuwa wakili wake amepata dharura hivyo hatoweza kufika Mahakamani hapo.

Aidha Hakimu Luborogwa alihairisha kesi hiyo hadi Oktoba 29 kwa ajili ya kuendelea, Idris na wenzake wanakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha Maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA).

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger