9/12/2020

Wasafi FM Yafungiwa siku 7 na TCRAMAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kusitisha utoaji huduma za utangazaji kwa Wasafi FM kwa muda wa siku saba baada ya kukiuka kanuni za utangazaji kwa kutumia lugha za matusi kwenye kipindi cha The Switch na Mashamsham.Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa tarehe 11 Septemba 2020 jijini Dar es Salaam, amewataka Wasafi FM kutumia siku nzima ya leo kuomba radhi kutokana na ukiukwaji huo wa kanuni kwa kutumia lugha za matusi ambazo hazikubariki.Kilaba amesema, adhabu hiyo itaanza kutumika kesho Jumamosi tarehe 12 hadi 18 Septemba 2020 na endapo Wasafi FM hawatatekeleza adhabu hiyo, TCRA itachukua hatua kali zaidi.James Kilaba, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Mkurugenzi mkuu huyo, ametoa wito kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kutumika kuonyana ili kunusuru adhabu hizo ambazo hawapendi kuzitoa.

Adhabu ambayo wameipata Wasafi FM inafanana na walioipta Clouds Televisheni na Clouds Redio ambazo TCRA iliifungia kwa siku saba kuanzia tarehe 28 Agosti hadi 3 Septemba 2020

Pia, TCRA ilitaka Clouds kutumia vituo vyake kuomba radhi tarehe 27 Agosti 2020 kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji kupitia kipindi cha Clouds 360.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger