9/14/2020

Zitto Kabwe Adai ACT Wazalendo Ipo Tayari Kushirikiana na Chadema...Hatma ya Bernard Membe Bado Haijulikani


Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema chama chake kipo tayari kushirikiana na CHADEMA kwa kuungana kwa wagombea wanaokubalika kwenye majimbo

Alitoa ufafanuzi baada Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu, kuomba kuachiwa kugombea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa wao wamemuachia Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo-Zanzibar, kwa kuwa ndiye anayekubalika

Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo, Bernard Membe, bado hajaongea chochote kuhusu hilo hata alipotafutwa kwa simu alikuwa hapatikani na alivyotumiwa ujumbe mfupi kupitia WhatsApp hakujibu

Aidha, Septemba 8 Membe aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa hatajiondoa kwenye kinyang’anyiro cha Urais, na kuahidi kuja na kimbunga kuanzia Septemba 15
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger