10/11/2020

Kauli ya LeBron kuhusu mashabiki wa LakersNyota wa mchezo wa mpira wa kikapu, LeBron James ameweka wazi somo ambalo amejifunza kutoka kwa mashabiki wa Los Angeles Lakers, kuwa hawajali wasifu wa mchezaji hadi atakapowaletea ubingwa wa NBA.

LeBron ambaye alitwaa ubingwa wa NBA mara tatu akiwa na timu tofauti, alisema kutwaa ubingwa kwa Lakers ndio njia pekee ambayo anaweza kupata kiwango kipya cha heshima kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo huko Los Angeles.


''Nilichojifunza kwa mashabiki wa Los Angels Lakers ni kwamba hawatojali wasifu wako kwa ulichokifanya awali, watakupa heshima iwapo utawapelekea ubingwa'', amesema LeBron James.


Los Angeles Lakers inaongoza fainali kwa 3-1 dhidi ya Miami Heat na huenda ikatwaa taji la ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10, iwapo itashinda mchezo wa tano alfajiri ya Oktoba 10, 2020.


Ikumbukwe LeBron alikuwepo kwenye kikosi cha Cleveland Cavaliers kilichotoka nyuma kwenye kipigo cha 3-1 na kuibuka mabingwa mwaka 2016 dhidi ya Golden State Warriors.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger