11/10/2020

Dkt. Abbas Awashukia Chadema, Ajibu Hoja Zao "Wanafanya Maigizo"MSEMAJI Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa Watanzania wamemaliza uchaguzi na sasa wanaendelea na michakato ya kidemokrasia, kisheria na kikatiba ya kujenga taasisi za nchi ili kazi iendelee na kamwe hawapotezi muda na kile alichokiita “maigizo” ya baadhi ya viongozi wa upinzani hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


 


“Hivi ninavyoongea na wewe mchakato unaofuata ni bunge kuanza, watachagua spika, watapelekewa jina la waziri mkuu kumthibitisha na kisha rais atazindua bunge, hao walioshindwa uchaguzi na kuanza tuhuma ni maigizo yao ambayo tumeyazoea kila mara wanaposhindwa,” amesema.


 


Akijibu mahsusi madai ya baadhi ya viongozi wa Chadema kama Tundu Lissu na Godbless Lema kuhofia usalama wao na hata kujaribu kuomba hifadhi ya ukimbizi nje ya nchi  Abbasi alishangazwa na madai hayo na kuhoji wametishiwa usalama wao na nani, wapi na lini?


 


“Mkataba wa Kimataifa wa Mwaka 1951 unaohusu Haki na Hadhi za Wakimbizi kwa mfano unaainisha bayana taratibu za kuwa mkimbizi, huwezi kuamka asubuhi tu ukajitangaza wewe ni mkimbizi au una kesi ya jinai ukataka kukimbia nchi kisa kudai ukimbizi.


 


“Mtu anaibuka anadai ametishiwa maisha lakini juzi tu katoka kushiriki kampeni siku 60 na amelindwa salama kabisa leo kashindwa anakwambia anahofia maisha. Mkimbizi gani anavuka mpaka mbele kaandaliwa gari ya kumchukua? Haya ni maigizo,” alisema.


 


Amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuenzi misingi ya amani na kuwataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi, anayehofu usalama wake atoe taarifa kwenye vyombo vya dola na amewataka wananchi kuachana na maneno ya watu waliokosa kuaminiwa na umma sasa wanatafuta kuonewa huruma.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

3 comments:

 1. Gud Moning Dkt Abbasi & DDC .

  Swadakta, Hawa ni Wasanii Next Level.


  Ruzuku is A Faru Joni Domain.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Infact, last year , we nominated them as contestants for 2025 Mlimani City primary entrants for the Oska Best Ever Movies

   Best Script
   Best Theme
   Best Characters
   Best Actors
   Best Sound effects
   Best Background scenes
   Best Location creation
   Best Vibekos of All times
   Best Creators of Matukio

   Above all.
   Faru Joni Ruzuku Control Domain.

   Kuna tetesi Shamba la Mahenge wamepelekwa wawekezaji na yule nanihi anataka kuwauzia sijui ubia..?? Asije kuwazidi kete Vibeko wenzake. Ruzuku is a call of the Day.

   All the Best for anticipated participation .

   Delete
 2. Mwenye kwao. Karudi kwao..

  Leo ni siku yetu Watanzania kujua
  mzalendo na kibaraka mkazi tofauti yao
  baada ya kushinndwa na uhamsishaji
  wa Jaribio la kuvunja Amani yetu.

  Aondoka kama kibaka

  ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger