11/07/2020

Georgia Kuhesabu Tena Kura za Urais
WAZIRI wa Masuala ya Kigeni katika Jimbo la Georgia, Brad Raffensberger, ametangaza kwamba jimbo hilo litahesabu upya kura zake za urais.


 


Amesema kura 4,169 hazijahesabiwa na kwamba kura 8,000 za wanajeshi bado zimo katika barua na kwamba sitahesabiwa zitakapowasili mwisho wa siku.


 


Siyo muda mrefu sasa, usiku kucha , Joe Biden amempiku Donald Trump katika mji wa Georgia. Na huku matokeo ya kura yakitolewa, Biden amechukua uongozi dhidi ya Trump katika jimbo la Pennsylvania.


 


Georgia yenye wajumbe 16 inatosha kumfanya Biden kupata matokeo sawa na Trump katika idadi ya wajumbe, huku akisubiri matokeo mangine kutoka majimbo mengine. Pennsylvania itamfanya Biden kuingia katika Ikulu ya Whitehouse.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger