Kaka wa Rapa 21 Savage Ameuawa kwa Kuchomwa Kisu Mjini London


Kaka wa rapa 21 Savage ameuawa kwa kuchomwa kisu mjini London. Terrell Davis mwenye umri wa miaka 27 alichomwa kisu hadi kufa kufuatia majibizano na rafiki yake juzi Jumapili (November 22) umeripoti mtandao Daily Mail.

21 Savage amethibitisha taarifa hizo kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, "Nashindwa kuamini kama kuna mtu amechukua uhai wako Kaka yangu, najua nimechukua hasira zako natamani ningerudisha muda." aliandika 21 Savage.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments