Mke wa Msanii Ali Kiba Afunguka Kuhusu Video ya Mahaba ya Nandy na Mumewe Ali Kiba

 


Mke wa msanii @officialalikiba, Aminah ametoa neno lake juu ya kilichofanyika kwenye ushirikiano wa mumewe wake na mwimbaji @officialnandy kwenye wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la "Nibakishie"


Wakiuvaa uhusika kwenye video ya wimbo huo, kuliibuka hisia tofauti kufuatia maigizo ya wawili hao walioamua kuutendea haki uhusika wa kilichoimbwa kama wapenzi wanaofurahia penzi.


Akijibu maswali ya wanaomfuatili kwenye ukurasa wake wa Instagram, Bi. Aminah ama @aileenalora kama ambavyo anatambulika mtandaoni, alirejesha jibu la swali lililouliza amepokeaje wimbo mpya wa #Nandy na #Alikiba maana yaliomo katika video yake ni makubwa kama mobimba, #Amina alijibu kuwa ameupokea kama ulivyo.


Sambamba na hilo, #Aminah pia alijibu swali la shabiki mwingine aliyemuuliza, Anajisikiaje kumuona mumewe anafanya video na wanawake wengine zisizo na maadili. Aminah alijibu swali hilo kwa ufupi kwa kumwambia Shabiki huyo, Aaangalie kazi kwanza mambo mengine baadae.


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments