Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mtoto mkubwa wa rais Trump aambukizwa virusi vya corona
Mtoto wa kwanza wa rais wa Marekani aitwaye Donald Trump Jr. yuko karantini tangu jana Ijumaa baada ya kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.
 Hayo yameelezwa na msemaji wa familia ambaye amearifu kuwa mtoto huyo wa rais Donald Trump hana dalili za kutisha za COVID-19 na kwamba anaendelea kwa kuzingatia ushauri wa kitabibu. 

Trump Jr mwenye umri wa miaka 42 anakuwa mtu wa hivi karibuni kabisa kutoka familia ya rais Trump kuambukizwa virusi vya corona ambavyo tayari vimewauwa zaidi ya watu 250,000 nchini Marekani na wengine milioni 12 wameambukizwa. 

Rais Trump mwenyewe, mkewe Melania na mtoto wao wa mwisho Baron walipona COVID-19 baada ya kuambukizwa mwezi Oktoba. 

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amesema suala la kukabiliana na janga la viruis vya coorna litakuwa kipaumbele cha utawala wake katika wakati rais Trump analaumu kwa kuchukua hatua za kusuasua kudhibiti kusambaa kwa maradhi hayo.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments