Nandy Bize Hadi Pumzi InakataSexy lady anayekimbiza kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’, amefunguka kuwa yupo bize sana na kazi yake ya muziki kiasi ambacho muda mwingine pumzi inakata.


Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Nandy ambaye anakimbiza na ngoma ya Dozi amesema kuwa, amekuwa bize na shoo kiasi cha kukosa hata muda wa kuingia mitandaoni kama ilivyokuwa awali.


“Nafanya kazi sana ninekuwa na shoo nyingi, muda mwingine nakosa hata muda wa kuposti mitandaoni maana huwezi kuposti kila kitu naamua nitulie tu.


“Sipumziki kiasi inafikia hata pumzi inakuwa ya shida na sio kwa sababu ya mwili wangu kuongezeka kama wana vyosema masha biki,” alisema Nandy. 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE