11/16/2020

Wafuasi wa Bobi Wine watawanywa kwa vitoza machozi Uganda


W


afuasi wa mgombea urais ambaye pia ni mwanamuziki Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, wamerushiwa vitoza machozi na polisi Jumapili nchini Uganda, pamoja na kumkataza mgombea huyo kuingia kwenye eneo alilopanga kufanya kampeni.

Wafuasi wa Bobi Wine walikuwa wamekusanyika katika mji wa Kumi, mashariki mwa nchi hiyo walipotawanywa.


Msafara wake baadaye ukakatazwa kuingia katika eneo la Sironko na kulazimika kurejea mji wa Mbale ambapo wafuasi wake walifyatuliwa vitoza machozi.


Bobi Wine aliweka picha za makabiliano kati ya polisi na wafuasi wake kwenye mtandao wa Twitter:


Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi miongo mitatu anatafuta kuchaguliwa tena.


Pia miongozo ya wizara ya afya inapinga wanasiasa kukusanyika na makundi makubwa ya wafuasi yao, badala yake, kuhutubia umati wa watu usio zidi 70.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger