China yamfunga Mwanahabari Aliyetangazia Mlipuko wa kwanza wa Virusi vya Corona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwnahabari wa Chiana aliyeangazia mlipuko wa kwanza wa virusi vya corona katika mji wa Wuhan amefungwa miaka minne jela.

Zhang Zhan alipatikana na kosa la "kuanzisha uvumi na kuzua vurugu", mashataka mara kwa mara dhidi ya wanaharakati.


Wakili huyo wa zamani aliye na umri wa miaka 37 aliyezuiiwa mwezi Mei, amegoma kula kwa miezi kadhaa. Mawakili wake wanasema afya yake imedhoofika vibaya.


Bi. Zhang ni mmoja wa wanahabari kadhaa raia wa China waliojipata mashakani kwa kuripoti kuhusu mwenendo wa virusi vya corona katika eneo la Wuhan.


Hakuna vyombo huru vya habari nchini China na mmalaka inajulikana kwa kuwasaka na kuwachukulia hatua kali wanaharakati wanaoonekana kuhujumu juhudi zaa serikali kukabiliana na mlipuko huo.


Bi Zhang aalifikishwa katika mahakama ya Shanghai akiwa na wakili wake Jumatatu asubuhi.


Kwa mujibu wa mashataka yanayomkabili, alisafiri hadi Wuhan mwezi Februari kuripoti kuhusu mlipuko wa virusi bila kuzingatia kanuni zilizowekwa.


Ripoti yake aliyoweka mubashara katika mtandao wa kijamii ilivuma sana mwezi Februari, ilimweka mashakani baada ya kuvutia mamlaka za China.


Mtandao wa China wa kutetea haki za binadamu ulisema ripoti zake zilijumuisha habari za kuwekwa kizuizini kwa waandishi huru wa habari na unyanyasaji wa familia za wahanga ambao walikuwa wakitafuta uwajibikaji.


Japo ni nchi ambayo ilikuwa kitovu cha janga la corona, China sasa imeweza kudhibiti virusi vya ugonjwa huo


Bi Zhang alitoweka Wuhan mnamo Mei 14 kwa mujibu wa CHRD. Siku moja baadae, ilifichuliwa kwamba alizuiliwa katika kituo cha polisi cha Shanghai, zaidi ya kilo mita 640 kutoka hapo.


Alishtakiwa rasmi mwezi Novemba. Nyaraka za mahakama zinasema alitoa "taarifa za uonga kupiti aujumbe mfupi, video na kupitia [mitandao kama] WeChat, Twitter na YouTube".


Pia anatuhumiwa kwa kukubali kuhojiwa na vya vyombo vya habari vya kigeni "kueneza habari za uvumi" kuhusu virusi huko Wuhan.


Kifungo cha kati ya miaka minne na mitano kilipendekezwa kutolewa dhidi yake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad