Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Simba yaanza Mchakato wa Kumuongezea Mkataba Chama

IMEELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Simba, Clatous Chama kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na mabosi wa timu hiyo wakimshawishi aongeze mkataba mpya ndani ya kikosi hicho.

Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa wamefikia hatua nzuri ya mazungumzo jambo linalotoa matumaini kwa Chama kusaini mkataba mpya.

"Kwa sasa bado Chama hajasaini mkataba na amekuwa kwenye mazungumzo na viongozi ili aweze kusaini kwani ni mchezaji muhimu ndani ya kikosi.

"Imekuwa akitajwa kuwa kwenye mazungumzo na Yanga jambo linalowapa presha viongozi hasa ukizingatia ni mchezaji muhimu kikosi cha kwanza," ilieleza taarifa hiyo.

Hivi karibuni uongozi wa Simba uliweka wazi kwamba umemalizana na nyota huyo ambapo atabaki ndani ya kikosi hicho mpaka 2023 jambo ambalo linatajwa kuwa bado halijakamilika.

Mkataba wa Chama ndani ya Simba kwa sasa umebakiza miezi sita na anaruhusiwa kuzungumza na timu ambayo inahitaji huduma yake kwa mujibu wa kanuni za Fifa.

Ndani ya Simba kwa msimu wa 2020/21 amehusika kwenye mabao 12 kati ya 33 ambapo amefunga mabao sita na kutoa pasi sita za mabao.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments