Mke wa Boss Alivyompa Shavu Mwanamuziki StaminaMsanii wa HipHop hapa nchini Tanzania Stamina Shorwebwenzi kutoka kundi la Rostam siku ya leo ameweza kusainiwa kwenye lebo ya Akida OG chini ya Mkurugenzi na Boss wa lebo bwana Akida OG mwenyewe.


Boss Akida OG amesema ameamua kuchukua msanii huyo kwa sababu mke wake mkubwa anamfuatilia, kumpenda na kumtajataja sana na yeye kwakuwa anampenda mke wake akaamua kumsaini ili afanye naye kazi.


Tayari lebo hiyo ina jumla ya wasanii wanne kwa sasa ambao ni Rhino King, Mkali Wenu, Official Nai na Stamina Shorwebwenzi.


Kwa upande mwingine msanii wa BongoFleva Ommy Dimpoz amepata shavu la kusainiwa kwenye lebo kubwa Africa ambayo inajulikana kwa jina la 'Sony Music Africa' ambayo ipo nchini Africa ya Kusini.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments