Msanii wa Harmonize Ibraah Atangaza Kutoa Nyimbo Tatu Kwa Mpigo


Nyota mpya wa kizazi kipya chini ya lebo ya Konde Music Worldwide, #Chinga @ibraah_tz anatarajia kuachia ngoma zake tatu kwa mpigo, amezipa jina "Karata tatu" na zitatoka wiki ijayo.


Karata tatu imesheheni nyimbo kama "Mapenzi", "Upande" na "Nimpende". Kwenye wimbo namba mbili ambao ni "Upande", msanii @ibraah_tz amemshirikisha #Skales toka Nigeria, ambaye pia ni mwanafamilia wa @kondegang, ikiwa Lebo hiyo inamsimamia kazi zake kwa upande wa Afrika Mashariki.


Ikumbukwe, @ibraah_tz alisainiwa na Konde Music Worldwide, Aprili 11 mwaka huu na hadi sasa kueleka kuumaliza mwaka tayari ametoa nyimbo 8 pekee, ambazo ni (1) Nimekubali (2) Sawa, (3) Nani, (4) Subira ft Skibii, (5) Wawa ft Joeboy, (6) Wandoto, (7) One night Stand ft Harmonize na (8) Nitachelewa, huku nyimbo 3 zikitarajiwa kutoka wiki ijayo.


Jumla ya nyimbo zote kwa mwaka 2020, msanii @ibraah_tz atakuwa ametoa nyimbo 11. Tuachie ujumbe wako hapa kwa #Chinga, akipita atausoma.

That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments