Rais Trump Amshinikiza Gavana Kupindua Matokeo
Rais wa Marekani Donald Trump, amemshinikiza gavana wa Republican wa jimbo la Georgia kumsaidia kupindua ushindi wa Joe Biden jimboni humo.

 

Katika mfululizo wa ujumbe aliotuma kupitia mtandao wa Twitter, Rais Trump amemtaka mgombea Brian Kemp kuitisha kikao maalum cha bunge.

 

Hatua hiyo imekuja saa kadhaa baada ya Rais Trump kuhudhuria mkutano wa kampeni huko Georgia wakati jimbo hilo linajitayarisha katika marudio ya uchaguzi wa seneti.

 

Rais bado amekataa kukubali kuwa alishindwa katika uchaguzi mkuu akidai kulikuwa na wizi wa kura ingawa hajawahi kutoa ushahidi wowote kuthibitisha kwamba ushindi wa Biden ulitokana na wizi wa kura.

 

Trump amefungua kesi mahakamani katika majimbo kadhaa lakini hadi kufikia sasa zote zimeshindwa kufaulu.

 

Jimbo la Georgia lilikuwa ngome muhimu katika uchaguzi huo ambapo Joe Biden aliibuka na ushindi mdogo – ikiwa ni mara ya kwanza jimbo hilo linampigia kura mgombea urais wa chama cha Democrat tangu mwaka 1992.


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments