Sean Kingston Anaendelea Kunuka Madeni tu, Ashtakiwa Kwa Kushindwa Kumlipa Muuza Urembo


Sean Kingston anaendelea kunuka madeni tu, ameripotiwa kushtakiwa na muuza mrembo. Kingston ameshtakiwa kwa wizi mara baada ya kutomlipa muuzaji mmoja wa vito vya thamani.


Tovuti ya TMZ imeripoti kwamba rekodi za mahakama zinaonesha kwamba Kingston alifikishiwa mzigo huo lakini hadi leo bado hajafanya malipo.


Kumbukumbu zinaonesha kwamba hii imekuwa tabia ya mwimbaji huyo, mwaka 2017 alishtakiwa kwa kushindwa kulipia gari alilouziwa, miezi michache baadaye muuzaji wa vito vya thamani alimshtaki kwa kushindwa kulipa deni la Saa aina ya Rolex, alishindwa kesi hiyo na alitakiwa kumlipa muuzaji huyo ($300K) takribani TSH. 695M

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments