Watu karibu 700 wafa kwa COVID-19 Ujerumani


Watu 698 wamekufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19 kwa muda wa saa 24 zilizopita nchini Ujerumani, hii ikiwa ni kulingana na taasisi ya Robert Koch inayoshughulikia magonjwa ya kuambukiza nchini humu. 
Idadi hiyo ni ya pili kwa ukubwa kurekodiwa kwa siku moja tangu mripuko wa maradhi hayo kuwasili Ujerumani. 

Ujerumani pia imerekodi visa vipya vya maambukizi ya corona 26,923 katika muda wa saa 24 zilizopita, ilikiwa ongezeko la visa 48 ikilinganishwa na siku iliyotangulia. 

Kwa ujumla, Ujerumani ambayo tangu Jumatano imeimarisha masharti ya kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya corona, imepoteza watu 24,125 kwa maradhi ya COVID-19. 

Huku hayo yakiarifiwa, mawaziri wa afya katika majimbo yote 16 ya Ujerumani wanakutana kukamilisha mipango ya kuanza kutoa chanjo ya ugonjwa huo kote Ujerumani kuanzia tarehe 27 mwezi huu wa Desemba.

Wakati huo huo, taarifa za hivi punde zimearifu kuwa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekutwa na mambukizi ya virusi vya corona.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments