Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Hivi Unajua Donald Trump BADO Hajakubali Kushindwa Urais Marekani...Anapambana ya Hela Otee Matokeo Yabadilishwe


Rais wa Marekani, Donald Trump amerekodiwa akimwambia Afisa Mkuu wa Uchaguzi jimbo la Georgia atafute kura za kutosha kuwezesha kubadilishwa kwa matokeo ya uchaguzi.


"Nataka tu kupata kura 11,780," amenukuliwa Trump akimwambia Katibu wa Chama cha Republican, Brad Raffensperger jimboni humo katika mazungumzo yaliyorekodiwa na kutolewa na gazeti la Washington Post.


Katika mazungumzo hayo, Raffensperger anasikika akijibu kuwa matokeo ya uchaguzi ya Georgia yalikuwa sawa.


Raid mteule, Joe Biden alishinda uchaguzi wa Georgia pamoja na majimbo mengine muhimu na kumuwezesha kupata kura 306 za wajumbe dhidi ya Trump aliyepata kura 232.


Tangu uchaguzi mkuu wa Novemba 3, Trump amekuwa akidai kuwa kura ziliibwa bila kutoa ushahidi wowote unaothibitisha madai yake.


Tayari majimbo yote 50 yamethibitisha matokeo ya uchaguzi huo baadhi ya vituo ikiwa ni baada ya kura kuhesabiwa tena au pia kwa sababu ya kesi zilizowasilishwa mahakamani kupinga matokeo.


Hadi kufikia sasa, Marekani imetupilia mbali kesi 60 zilizokuwa zimewasilishwa kupinga ushindi wa Biden.


Aidha, bunge linatarajiwa kuidhinisha rasmi matokeo ya uchaguzi huo Jumatano ya Januari 6.


Bwana Biden wa chama cha Democrat, anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Marekani Januari 20.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments