Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Jamaa Amefukuzwa Kazi Kwa Kumsema Mama yake Vibaya Mbele ya Boss


Jamaa mmoja nchini Nigeria amefukuzwa kazi mara baada ya kutoa kauli kuhusu Mama yake mzazi, kauli ambayo haikumfurahisha Boss wake.


Kijana huyo ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye ofisi ya masuala ya PR, alikuwa akizungumza na mwajiri wake kwa njia ya simu huku akiwa amesimama pembeni ya mama yake mzazi. Mwajiri wake alisikia sauti ya mama wa kijana huyo na kuomba amsalimie.


Kabla Kijana huyo hajampatia simu Mama, alimwambia mwajiri wake kuwa "Mama yangu hana elimu (illiterate) tafadhali zungumza naye Kiyoruba. Baada ya kauli hiyo, mwajiri wa kijana huyo alikasirika kusikia hivyo na na kusema "Unathubutu vipi kumuita Mama yako mtu asiyejua kusoma na kuandika, hivi ndivyo huwa unachafua sura za wateja wetu pia."

-

Baada ya hapo Boss huyo alikata simu na kilichofata nikuandika email na kumfukuza kazi Kijana huyo. Nini maoni yako?

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments