Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Marioo Magari Kama Yote

BAHATI ya mtu usiilalie mlango wazi. Wasanii wengi wamepata mafanikio makubwa baada ya kudumu muda mrefu kwenye gemu lakini kwa upande wa Omari Mwanga ‘Marioo’ mambo ni tofauti, amefanikiwa kumiliki magari makali ndani ya muda mfupi tu!

 

Kinachofurahisha zaidi, bwa’mdogo huyu hana tambo, mbwembwe, wala makekeme mengi, lakini anakimbiza mwizi kimyakimya na kufanya muziki wake mzuri.

 

Taarifa ikufikie kwamba, Marioo kwa sasa anatamba na ndinga kali tatu kwa mpigo, na hii ni kutokana na matunda ya muziki wake anaoufanya.

Marioo anamiliki BMW, Subaru Impreza na Toyota Land Cruiser Prado aliyozawadiwa na kampuni ya JCW.

Ukiachilia mbali na magari hayo anayoyamiliki lakini pia ameweza kutaja gari ambalo ni gari la ndoto yake ni BMW-X6.

 

MASHABIKI WAMWAGIA SIFA

Kama tunavyofahamu watu wa kwenye mitandao ukifanya kitu kibaya wanakusema lakini pia ukifanya kitu kizuri huwa wanakusifa, mashabiki wameonekana kupendezwa na vitu ambavyo anafanya mkali huyu.

 

“Msanii ndiyo unatakiwa kufanya mambo kama haya bhana siyo kila siku unafanya muziki na hatuoni maajabu yoyote, Marioo ni kijana mdogo sana lakini anafanya vitu vikubwa sana kura zangu zote nampa Marioo,” achangia shabiki mmoja aliyejiita kikaa _masai kwenye ukurasa wa Instagram.

 

HUYU HAPA MARIOO…

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilipiga stori mbili tatu na msanii huyo ambapo alisema kuwa, anapenda sana kununua magari na kuwa na maisha mazuri.

“Nafanya kazi ngumu sana nalala muda mchache, kwa nini nikipata pesa nisizitumie kwa vitu ambavyo navipenda? Kiukweli mimi napenda sana kuwa na maisha mazuri, kingine napenda sana magari ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu.

 

“Ila kwa kiasi chake Mungu ameweza kunitendea, namshukuru sana Mungu na mashabiki wangu maana bila sapoti yao wala mimi nisingekuwa hapa nilipo, nawapenda sana mashabiki wangu,” alisema Marioo.

 

Kwa hatua kubwa aliyoweza kupiga msanii huyo kwa kupata mafanikio kama haya, kwa sasa ameweza kuungana na wasanii wengine wenye mafanikio kwenye muziki kama Nasibu Abdul “Diamond Platnumz’ Rajabu Abdul ‘Harmonize’, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ na Ali Salehe Kiba ’Alikiba’.

 

Mario hajafikisha hata miaka mitano kwenye gemu lakini amekuwa na mafanikio makubwa kwenye nyimbo zake kali kama vile Inatosha, Chanda Chema aliomshirikisha Darassa na Mama Amina.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments