Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Matokeo ya Uchaguzi Uganda 2021: Yoweri Museveni bado anaongozaNi siku ya pili kura zikiwa zinaendelea kuhesabiwa, raia wa Uganda walipiga kura Januari 14 ambapo rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 35 amekuwa akichuana vikali na mwanasiasa aliyekuwa mwanamuziki Robert Kyagulanyi almaarufu kama Bobi Wine, Na sasa zaidi ya 86% ya kura zimehesabiwa.


Bwana Museveni, 76, anaongoza kwa kura 5,303,831 ambapo ni sawa na (58.83%) huku mpinzani wake, Bobi Wine akiwa na kura 3,119,965 (34.62%) kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Uganda.

Download App ya Udaku Special HAPA Kusoma Hizi Habari Kupitia Simu yako Kirahisi


Awali , mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Simon Byabakama alisema kuwa upigaji kura ulienda kwa amani, na kusifu mafanikio hayo.


Matokeo hayo yamekuwa yakitangazwa licha ya kuzimwa kwa mtandao, alisema.


 "Hatutumii intaneti ya ndani ya nchi kutangaza matokeo. Tunatumia mifumo yetu wenyewe. Msiwe na hofu na matokeo licha ya kwamba hakuna intaneti," aliwaambia waandishi.


Lakini Bobi Wine, alisema baadhi ya wawakilishi wake katika vituo vya kuhesabia kura walikamatwa Alhamisi, na anaamini kuwa kuzimwa kwa mintaneti kumetumika ili kuvuruga uhesabuji wa kura.


Vilevile ni kama mawasiliano yote yamekuwa na shida kwa sababu watu wamekuwa na wakati mgumu kutuma ujumbe mfupi pia.


"Ningefurahi kuwashirikisha video za udanganyifu na kutofuatwa kwa utaratibu lakini mpaka intaneti irejeshwe," Reuters ilimnukuu Bobi Wine.


Tume ya Uchaguzi inasema ni vituo viwili tu katika nchi nzima ndivyo vimeripotiwa kuwa na chagamoto na zoezi la upigaji kura lilifutwa.


Mwandishi wa BBC anasema ulinzi ni mkali na vikosi vya usalama vinafanya doria katika mji mkuu wa Kampala.


Mji umekuwa kimya na baadhi ya maduka yakiwa bado yamefungwa, AFP imeripoti.


Vikosi vya usalama vilianza kukabiliana na mikusanyiko ya watu kabla ya uchaguzi na makumi ya watu wakauawa.


Serikali imesema marufuku ya kukusanyika ilikuwa inalenga kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona huku upinzani ukisema ilikuwa hatua ya kuwakandamiza.


Bobi Wine na wengine kati ya wagombea 10 wa upinzani wamekamatwa katika matukio mbalimbali - wakati wa maandamano yaliyosababishwa na kukamatwa kwa mmoja wao mnamo mwezi Novemba, ambapo watu zaidi ya 50 walipoteza maisha yao.


Bwana Museveni, ambaye aliingia madarakani kwa kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka 1986, anawania kuchaguliwa tena kupitia chama cha National Resistance Movement (NRM).


Kwa muda mrefu amekuwa akichukuliwa na raia wa Uganda kama mkombozi na mletaji wa amani.


Bobi Wine inasemekana ndiye mgombea mpinzani mkuu kati ya wagombea 10 wa upinzani katika kinyang'anyiro hicho cha urais.

Download App ya Udaku Special HAPA Kusoma Hizi Habari Kupitia Simu yako Kirahisi


Nyota huyo wa muziki aina ya Reggae anafahamika na wafuasi wake kama rais wa ghetto.


Kampeni za chama chake cha National Unity Platform (NUP) zilikuwa zimelenga mahitaji ya msingi kama kuimarisha huduma ya afya, elimu, maji safi na upatikanaji wa haki.


Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, muziki wa Bobi Wine umekuwa ukiangazia masuala hayo na kutia moyo wafuasi wake.


Amekulia katika kitongoji duni cha Kamwokya mjini Kampala ambako pia amejenga studio maarufu duniani. Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

2 Comments

  1. Naona mmeamua kubadilisha template.
    Sawa tupo pamoja

    ReplyDelete
  2. Basi nichukue fursa hii kuwakaribisha katika ULIMWENGU WA FASIHI. Karibuni katika blog yangu kwa makala mbali mbali zikiwemo AFYA, TEKNOLOJIA na Mambo mbali mbali

    www.mrbunduki.com

    ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)